Wakati huo huo, Miji tofauti ya Pakistan pia ilishuhudia utekelezaji wa Sala ya maiti ya bila kuwepo kwa Shahidi huyu Mujahid, na kuwepo kwa makumi ya maelfu ya wafuasi wa Palestina.
Maadhimisho ya siku ya maombolezo ya umma katika ngazi ya Kitaifa, kuidhinishwa kwa azimio la kuiunga mkono Palestina, kulaani mauaji ya Shahidi Haniyeh na vitendo vya kigaidi vya utawala ghasibu wa Israel katika Bunge la Pakistan; ni miongoni mwa matukio mengine yaliyo nchini humo hii leo.